logo

POLISI IRINGA YAPOKEA PIKIPIKI 10 ZA KISASA TOKA KWA WADAU

JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa limepokea msaada wa pikipiki 10 za kisasa zenye thamani ya shilingi milioni 55 kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Iringa.

Akizungumza katika halfa hiyo ya makabidhiano ya pikipiki hizo Jana Juni 27, 2023 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amewapongeza wadau kutoka sekta binafsi kwa kutoa vifaa vya usafiri kama sehemu ya kupanua wigo wa mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu pamoja na kurudisha fadhila kwa Jamii.

Kwa upande wa baadhi ya wadau waliofanikisha zoezi hilo ikiwa Kampuni ya ASAS, EAST AFRICAN BORNWOOD , YISEN INTERNATIONAL INVESTMENT wakizungumza katika hafla hiyo wamesema kuwa lengo la kutoa mchango huo ni kutambua mchango wa Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa wananchi.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Allan Bukumbi amesema kuwa kwasasa tunaendelea na zoezi la utoaji mafunzo kwa Askari watakaotumia pikipiki hizo ili kutambua matumizi sahihi na utunzaji wa vyombo hivyo.

Aidha,Bukumbi amewashukuru wadau mbalimbali kwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuleta maendeleo na kuonesha jitihada katika kuzuia uhalifu.
@polisi.tanzania
#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn