DKT.MPANGO AITAKA JKT KUWAFUNDISHA VIJANA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA SHUGHULI ZAO
MAKAMU wa RAIS Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango Amelitaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuwekeza Zaidi Katika Kufundisha Vijana Matumizi ya Teknolojia Katika Shughuli zao Mbalimbali za Uzalishaji Mali na Utoaji Wa Huduma Kwa Wananchi.
Dkt.Mpango Ameyasema Hayo Leo Julai 1,2023 Alipokuwa Akifungua Wiki ya Maonesho Kuelekea Kilele Cha Miaka 60 Ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Tukio lililofanyika Katika viwanja vya SUMA JKT House Jijini Dodoma.
Zama Hizi Sio Zama za Kutumia Misuli, Bali Akili Zaidi Na Teknolojia Zaidi"amesema Dkt.Mpango
.
Aidha amesema ni Vema Jeshi Hilo lifikirie Namna Ya kuwatambua wataalamu wake Wabunifu na kuwapatia Tuzo, Na Jambo Hilo lifanyike Kwa Kushirikiana na Taasisi Husika Serikalini Hususani Kuwa na Hakimiliki Ya Ubunifu na Gunduzi Mbalimbali zinazofanywa Katika JKT.
.
"Napenda Kulikumbusha Jeshi la Kujenga Taifa liongeze Msukumo Katika Kuibua,kukuza na Kuendeleza Vipaji Katika Michezo, Music, Sanaa Na Utamaduni. Napenda Nitoe Pongezi Kwa Timu zetu za JKT ambazo zinafanya Vizuri Katika Maeneo Mbalimbali" Amesisistiza Dkt. Mpango.
.
Makamu Wa Rais Huyo Ametumia nafasi hiyo kulipongeza JKT kwa shughuli inazofanya za uzalishaji Mali hasa kwenye kilimo huku akisema linaweza kuwa fursa ya kufanya nchi ya Tanzania kuwa ghala la chakula.
"Naamini Jeshi Hili Lina Uwezo Kuwa Chachu ya kuifanya Tanzania Kuwa Ghala ya Chakula Hivyo naomba Uongozi Wa JKT Kubuni Mbinu Mpya za Kuchagiza Agenda Ya Kuifanya Tanzania Kuwa Ghala ya Chakula Katika Ukanda Wa Bara la Africa na Hata Pande zingine za Dunia.
.
Dkt.Mpango Amesema Juhudi za Kupanda Miti na Kutunza Mazingira zifanyike Katika Kambi Zote za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hapa Nchini Kwani Ikifanyika Hivyo Tutahakikisha Mazingira Yetu yanatunzwa Kwa Faida Ya Kizazi hiki na Vizazi Vijavyo.
.
Aidha, Mpango Ametoa Rai Kwa Wananchi Wote Wa Mkoa Wa Dodoma na Mikoa Jirani Kujitokeza Kwa Wingi Katika wiki Nzima Ya Maadhimisho Ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
.
Kwa Upande Wake Waziri Wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe.Innocent Bashungwa Amesema Kupitia Maadhimisho Hayo JKT itatumia Wiki Hii Kuelezea Na kuonesha Wananchi Kazi zake Na Malengo Yake.
.
Bashungwa Amesema Wizara yake na JKT Itaendelea Kushirikiana na Wizara Za Kisekta Katika Kuboresha Mafunzo ya Stadi za Kazi Kwa Vijana Wa JKT Na kuwawezesha Kwa kuwapatia Ujuzi na Maarifa Zaidi ya ilivyo Sasa kama alivyopewa Maagizo na Makamu Wa Rais Ili Baada ya kuhitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa waweze Kujitegemea Kwa Kuanzisha Shughuli Mbalimbali za ujasiriamali.
.
Naye Mkuu Wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele Amesema Tangu Kuanzishwa Kwa Jeshi Hilo Mwaka 1963 mpaka Sasa Hivi, JKT imetekeleza Majukumu yake ya Msingi Kwa Ufanisi Mkubwa Na Kufanikiwa kubadili Fikra za Vijana Kwa kuwajenga Katika Hali ya Umoja, Moyo Wa Kupenda Kazi, Uadilifu, Nidhamu, Uzalendo na Uelewano Bila kubaguana Kwa Misingi ya Dira, Udini, Jinsia na Kudumisha Uhuru na Amani ya Taifa
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

