MWENGE WAPITISHA MRADI WA MAJI IMBASENY MKOANI ARUSHA
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 kitaifa Abdallah Shaib Kaim amekagua na kuridhika na mradi wa maji wa Imbaseny, kata ya Imbaseny katika Halmashauri ya Meru, Arumeru.
Mradi huo umefanikishwa na Mamlaka ya Majisafi Arusha (AUWSA) unazalisha maji kiasi cha lita 2,594,000 kwa siku na kunufaisha wakazi zaidi ya elfu 19 wa vijiji vya Kiwawa,Ngongongare na Imbaseny. Thamani ya mradi ni kiasi cha shilingi 1,920,193,989.60 na mpaka sasa kiasi cha shilingi milioni 600,000,000 zimetolewa na Serikali na utekelezaji umefika asilimia 35, na mradi unatarajia kukamilika mwezi Disemba 2023.
Wakazi wa eneo hili hawajawahi kuona maji bombani katika makazi, hivyo Serikali ya Awamu ya Sita imewatua ndoo kichwani kwa maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Maji.
@wizarayamajitz
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

