MITINDO YA KUJAMIIANA YAWEZA KUVUNJA UUME
Utafiti wa madaktari wa idara ya Magonjwa ya Mfumo wa Mkojo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa imebainisha kuwa mitindo ya kujamiiana unaweza kusababisha uume uliyosimama kwa muda mrefu kuvunjika.
.
Utafiti wa madaktari hao umechapishwa kwenye Jarida la kimataifa la case za Upasuaji (International Journal of Surgery Case Reports, 108(2023)108415) wameripoti kufanya upasuaji wa kuunga uume wa kijana mwenye umri wa miaka 27 uliyovunjika wakati akijamiana na mkewe.
.
Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti huo, ajali ya kuvunjika uume si suala lenye kujitokeza mara kwa mara, linauwiano wa 1 kati ya watu 175,000.
.
Hata hivyo, utafiti huo unadokeza kuwa, tafiti zilizofanyika katika mataifa ya Ulaya na Marekani zimeonesha kuwa asilimia 93.3 ya ajali za uume hutokana na kujamiiana, ambacho kilikuwa chanzo cha ajali ya Uume aliyopata kijana aliyetibiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

