DORIS MOLLEL FOUNDATION YATOA VIFAA VYENYE THAMANI YA TSH.MILION 190 BUHIGWE KIGOMA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Mpango amepokea vifaa vyenye thamani ya Tsh.Milioni 190 kutoka kwa Taasisi ya Doris Mollel katika Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.
.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni vifaa tiba kwa ajili ya watoto njiti, Madawati 450 pamoja na mitungi ya gesi 300 kwa ajili ya Mama wajawazito na wahudumu wa Afya.
Katika hafla hiyo, Mpango ametoa rai kwa wadau mbalimbali nchini wakiwemo wanamuziki, wachezaji na hata waigizaji kuunga mkono jitihada za serikali katika kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti).
.
Ameipongeza Taasisi ya Doris Mollel ambayo imekuwa ikitekeleza shughuli zake kwa takriban miaka nane sasa katika kusaidia Serikali kutoa huduma kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati na pia kusaidia katika utoaji wa vifaa tiba vinavyotumika kuokoa maisha ya watoto hao.
Aidha, amekemea tabia za ukatili hususani kuwapiga wanawake wajawazito kwani madhara yake ni makubwa katika kupatikana kwa mtoto.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Bi. Doris Mollel amesema Taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na serikali katika jitihada za kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati pamoja na changamoto zinazopelekea kuzaliwa kwa watoto hao.
.
"Tayari taasisi Ya Doris Mollel Foundation kwa kushirikiana na wadau wengine tumefanikiwa kuhakikisha Bima Binafsi zinatoa huduma kwa mtoto anayezaliwa kabla ya wakati kupitia gharama ya Bima ya mama wa mtoto" Alisema Mollel.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

