logo

WAZIRI MKENDA AKAGUA MAANDALIZI YA UKARABATI CHUO KIKUU CHA MWL.JULIUS KAMBARAGE BUTIAMA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Julai 06, 2023 amekagua maandalizi ya ukarabati wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia kilichopo Butiama Mkoani Mara

Akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mtanga na Mbunge wa Jimbo la Butiama ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Jumanne Sagini wametembelea na kukagua maeneo yote ambayo yatafanyiwa ukarabati pamoja na kukagua vifaa vilivyonunuliwa kwa ajili ya kuanza ukarabati huo

Akizungumza mara baada ya ukaguzi Waziri Mkenda amesema chuo hicho kinapaswa kuanza kukarabatiwa ili kukiwezesha kudahili wanafunzi ifikapo Oktoba 2023 huku akiwataka kusimamia viwango na ubora .

Mkuu wa Mkoa wa Mara Said Mtanda amesema Mkoa wake utashirikiana na uongozi wa chuo hicho kuhakikisha ukarabati unakamilika kwa wakati.

Mbunge Jumanne Sagini amesema amefurahishwa kuona mizigo ya vifaa vya ukarabati kitu kinachompa faraja kwa kuwa anaona sasa Chuo kinaelekea kuanza kutoa mafunzo.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Bernard Melau amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ukarabati huo.

@wizara_elimutanzania

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn