RAIS SAMIA AITAKA USTAWI WA JAMII KUZINGATIA HAKI HASA KWENYE MATUNZO NA MASHTAKA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe,Dkt.Samia Suluhu Hassan Ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii Kuzingatia haki hasa kwenye Masuala Ya matunzo na mashtaka yanayowahusu watoto,na Yawepo mazingira rafiki kwao.
.
Samia Ameyasema Hayo Leo Julai 15,2023 Alipokuwa Jijini Dar Es Salaam Wakati Tume Ya Kuangalia Jinsi Ya Kuboresha Taasisi Za Haki Jinai Nchini ikiwasilisha Taarifa Yake.
.
Amesema Mapendekezo ya uboreshaji katika Haki Jinai yafanyike pande zote za Muungano ili haki kutendeka Sehemu Zote.
"Tushirikiane kuondoa rushwa, dawa za kulevya na mengine mengi tunayopaswa kuboresha kwa nguvu moja. Tutaunda Kamati zitakazoangalia kuhusu uhaba wa watumishi, ukosefu wa maadili, nidhamu na tatizo la rushwa kwenye vyombo vyetu vya utoajia haki na ukosefu wa ofisi katika ngazi za Wilaya kwa baadhi ya Taasisi zinazotekeleza Haki Jinai" Amesema Rais Huyo.
.
Kwa Upande Mwingine, Rais Samia Amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi Moses Kusiluka na Kamati iliyowasilisha ripoti leo ivunjwe vipande vipande viangalie mapendekezo yaliyotolewa ili kujua ya kufanyiwa kazi na Serikali moja kwa moja na yale yakubaki mikononi mwa kamati ili kufanyiwa utekelezaji kikamilifu na kwa wakati.
.
Aidha, Samia Amesema Kuhusu adhabu ya kifo na kifungo cha maisha, wataalam wayafanyie kazi na waje na mapendekezo kutokana na maoni ya Watanzania wanasemaje.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

