logo

KAIRUKI AKABIDHI MAGARI 25 KWA AJILI YA MAAFISA ELIMU

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki amekabidhi magari 25 ikiwa sehemu ya Magari 200 yaliyoagizwa kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) kwa ajili ya Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri zote nchini.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam katika hafla ya ugawaji wa magari hayo Mhe. Kairuki aliwataka GPSA

kukakamilisha upatikanaji wa magari mengine 105 yaliyosalia kwa ajili ya mafisa elimu hao.

"Katika Halmashauri 184 zinazotakiwa kupata magari, Halmashauri 51 tayari zimepata katika awamu ya Kwanza, awamu ya pili 19 na hii awamu ya tatu magari 25 hivyo bado magari 105 kwa maofisa hayo,"alisema.

Aidha, Kairuki ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha elimu na maslahi ya walimu nchini hivyo aliwataka maofisa hao wawe wabunifu kusimamia shughuli za Kieleimu na kuhakikisha kuwa Ubora wa Elimu unaimarika.

Kairuki amesema elimu sekondari inahitaji uwajibikaji na huwezi kupata mafanikio pasipo kuwa na ubunifu na bidii kwa watumishi hivyo Serikali inaendelea kuboresha na wasimamizi nao watekeleze wajibu wao.

Amewataka Maafisa hayo kutumia magari hayo kuongeza ufanisi wa shughuli za Kielimu na pia yatunzwe ili yaweze kudumu muda mrefu.

Vilevile aliwataka wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo kukazania masomo na kuepuka kuingia kwenye tabia zinazopingana na Mila na desturi za nchi.

Aliwataka wafuate mambo mazuri ya kizalendo yanayofundishwa na wazazi na walimu ili kukuza kiwango cha ufaulu.

"Akizungumzia kuhusu ujenzi wa bweni la watoto wa kiume kwenye shule ya Kibasila amesemk ni ahadi kutoka kwa Rais Dk.Samia kwa sababu alitaka kujua hitaji la shule hiyo na kutuelekeza sisi wasaidizi wake tulitatue na hivyo tunatekeleza agiza la Mhe. Rais.

Naye Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Abdul Maulid aliishukuruTAMISEMI kwa kutoa magari hayo kwani yamekuwa yakiwasaidia katika Ufuatiliaji wa elimu.

Pia aliipongeza serikali kwa kuwasikiliza hivyo ameahidi kwa niaba ya maofisa.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn