logo

DKT.NGAILO: UPATIKANAJI MBOLEA NCHINI UMEONGEZEKA KUTOKA TANI 543,043 HADI TANI 1,115,841

Mkurugenzi Mtendaji Wa Mamlaka Ya Udhibiti Wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt.Stephen Ngailo Amesema upatikanaji wa mbolea nchini umeongezeka kutoka tani 543,043 mwaka 2018/19 hadi tani 1,115,841 mwaka 2022/23, viwanda vya mbolea na visaidizi vyake nchini vimeongezeka kutoka viwanda vinne mwaka 2016/2017 hadi 17 mwaka 2022/23.

.

Ngailo Ameyasema Hayo Leo Julai 17,2023 Alipokuwa Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Kuhusu Utekelezaji Wa Majukumu ya Taasisi Hiyo Na Mwelekeo wa Mwaka 2023/24 Katika Ukumbi Wa Idara Ya Habari (MAELEZO) Jijini Dodoma.

.

Amesema Kutokana na kupanda kwa bei za mbolea katika soko la dunia, Serikali ilitenga fedha kwa ajili ya kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima kwa lengo la kupunguza gharama ya mbolea.

.

"Kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani" Amesema Ngailo.

.

Mkurugenzi Huyo Amesema Mbolea za kupandia na kukuzia zinahusika katika mpango wa ruzuku kulingana na mahitaji ambapo mfumo wa kidijitali unatumika kuratibu usajili wa wanufaika, usambazaji, mauzo na malipo ya fedha za ruzuku.

.

"Vipaumbele kwa mwaka wa fedha 2023/24 ni kuratibu na kusimamia utekelezaji wa utoaji wa mbolea ya ruzuku, kuratibu upatikanaji na usambazaji wa mbolea nchini takriban tani 850,000 na kuendelea kudhibiti ubora wa mbolea" Amesema Ngailo.

.

Aidha, Ngailo Amesema Kwa Mwaka Huu 2023/24 wamepanga kuhamasisha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha mbolea nchini, kushirikiana na wadau kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea na uimarishaji wa maabara ya uchambuzi wa mbolea.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn