KIPANGA:JIPANGENI KUTEKELEZA BAJETI ITAKAYOPITISHWA NA BUNGE
MENEJIMENTI ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeshauriwa kuwa na kikao kukaa kwa pamoja na zile za Taasisi zilizo chini ya Wizara ili kujipanga kwa pamoja kutekeleza bajeti itakayopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka wa fedha 2023/24.
Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga Jijini Arusha wakati wa kufunga mkutano wa 31 wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo.
Kipanga ameongeza kuwa ni muhimu kukaa na kukabiliana pamoja namna nzuri ya kutekeleza bajeti hiyo hasa fedha za miradi ya maendeleo kwa lengo ya kuwa na ufanisi na tija kwa maendeleo ya sekta ya elimu, sayansi, teknolojia na ubunifu.
“Ni muhimu na vyema kuwa na kikao cha pamoja ambacho baadhi ya wajumbe wa menejimenti kutoka taasisi zilizo chini ya wizara waje make pamoja na kupitiishana katika malengo, mikakati na vipaumbele vya wizara ili kuwezesha utoaji wa elimu bora itakayowasaidia wahitimu kushindana katika soko la ajira la dunia.
Aidha, amewataka wajumbe wa baraza hilo wanaporudi katika vituo vyao vya kazi kufanya kazi kwa weledi na ufanisi katika kuhakikisha wanafunzi, vijana na jamii wanahudumiwa vyema na hasa katika kusimamia miongozo, kanuni na sheria zinazotumika katika kuhakikisha elimu inatolewa katika mazingira bora.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo amemweleza Mhe. Naibu Waziri huyo kuwa wajumbe wa baraza hilo wamepata nafasi ya kupitishwa katika mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, mabadiliko ya Mitaala, utekelezaji wa masuala ya utawala na maendeleo ya utumishi na masuala yanayohusu afya ya akili kwa watumishi wa umma.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

