Top news
LUIS MIQUISSONE AREJEA RASMI SIMBA SC
Nyie watu! Simba wamerejesha homa na usumbufu kwa mabeki wa timu mbali mbali kwenye Ligi Kuu Bara na michuano mingine watakayoshiriki!
Pembezoni mwa mto Zambezi kuna mji unaitwa Tete ambao upo karibu na migodi ya makaa ya mawe!
Huu ni mji ambao katikati ya Karne ya 17 wareno waliufanya kuwa soko kuu la madini ya dhahabu na ndovu na tangu 1761 ulitambulika Rasmi kama mji wa kibiashara!
Wakazi wake wanaozungumza Kinyungwe, Kiingereza na Kireno ndio walizaliana na katikati ya kizazi hicho alizaliwa Luis Miquissone mnamo Julai 25, 1995. Bado siku 3 tu atimize 28π
Nyota wa zamani wa Mamelodi aliyetolewa kwa Mkopo Chippa United, Royal Eagles na UD De Songo kabla ya kutwaliwa na Simba ambako Afrika ilimtambua akiuzwa kwenda Al Ahly ya Misri... Anarudi nyumbani!
Mabibi na Mabwana... Luis Miquissone amerudi kuendelea kutoa sulubu! Wenzie wengi walioenda na kurudi mambo yamekuwa mazito!
Mwana wa Tete atatoa mwiru!? ππ
Wastue mabeki wawili waambie jamaa Karudiπ.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

