SIMBA SC KUMUUZA MCHEZAJI PAPE SAKHO KWA KLABU YA US Quevilly-Rouen Métropole
Klabu ya Simba imefikia makubaliano na klabu ya US Quevilly-Rouen Métropole ya Ufaransa ya kuuziana kiungo mshambuliaji Pape Sakho kwa ada mficho.
Klabu hiyo ni miongoni mwa klabu kongwe za Ufaransa ikiasisiwa 1902 na mafanikio makubwa inayojivunia ni kucheza fainali ya Kombe la Ufaransa 'Coupe de France' mwaka 1927.
Sakho anakuwa ni mchezaji wa 47 wa Afrika kusajiliwa na timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la Pili na msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya 11 kati ya timu 20.
Sakho atavaa jezi za Njano na Nyekundu akivua jezi Nyekundu na nyeupe za Simba ambako msimu uliopita alifunga mabao 9 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
All the best kipaji kikubwa kilichokosa mwendelezo mzuri! Sakho ni usajili mgumu zaidi kwa Marehemu Hans Pope!.
Pengo au mwanya pale Simba!?
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

