MEJA JENERALI MABELE: JKT TUMETENGEWA SHILINGI BILIONI 9.96 KUBORESHA MAKAMBI
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele Amesema Katika Bajeti Ya Mwaka Wa Fedha 2023/24 JKT imetengewa na Serikali Kiasi Cha Shilingi Bilioni 9.96 Kwa Ajili Ya Kuendeleza adhma ya Kuboresha na Kujenga Miundombinu Makambini.
.
"Katika Kipindi hiki tunaamini Kwamba Hizi Shiling Bilioni 9.96 tutaweza kuweka Miundombinu Mizuri Katika Makambi, Pamoja Na Kuhakikisha Kwamba tunaongeza Kambi zingine Ili Tuweze kuchukua Vijana wengi Zaidi" Amesema.
.
Meja Jenerali Mabele Ameyasema Hayo Alipokuwa akieleza utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/24 katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Julai 27, 2023 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.
.
Meja Jenerali Mabele Amewahasa Wananchi na Vijana wote Kwa Ujumla Kuhakikisha Kuwa, wanazitumia Fursa zinazopatikana za Kujiunga Na Mafunzo ya JKT kwani Jeshi la Kujenga Taifa Ni Sehemu Sahihi Kabisa.
.
"JKT ni Mahala Salama pa Kuwajengea Vijana Wetu Utaifa, Kwa Kuwalea Pamoja, Pasipo kujali Dini, Jinsia, Elimu au Kabila" Amesema Meja Jenerali.
.
Kwa Upande mwingine, Meja Jenerali Mabele Ameziomba Taasisi Za Umma Na Binafsi Kuona Umuhimu Wa Watendaji wao Ambao hawakupata Fursa Ya Mafunzo ya JKT, waweze Kufanya hivyo Kupitia Mafunzo ya JKT Kwa Makundi Maalum.
.
.
Meja Jenerali Huyo Amesema Pia wanaendelea Kuboresha Vyuo Vya Ufundi Stadi(VETA) Katika makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa hapa Nchini.
.
"Tumeongeza Chuo Kimoja Cha VETA Katika Mkoa Wa Kigoma, Kipo Chini Ya Kikosi Cha 824 Kanembwa, Kibondo" Amesema.
.
Aidha, Kwenye Upande Wa Kilimo Meja Jenerali Mabele Amesema wamekuja na Mkakati Ifikapo Mwaka 2024/25 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) liwe Lina Uwezo Wa kujitosheleza Kwa Chakula Hasa Katika Mazao yale ambayo yanaweza yakapatikana Shambani.
.
Kwa Upande Wake Msemaji Mkuu Wa Serikali Ndg.Gerson Msigwa Amesema JKT Ni Kimbilio Sio Sehemu Ya Kukimbia hivyo Vijana wote wanapaswa Kujiunga na Jeshi Hilo Ili waweze Kujifunza mambo Mbalimbali.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

