Top news
WAZIRI AWESO ARIDHISHWA UJENZI WA JENGO LA WIZARA YA MAJI MTUMBA JIJINI DODOMA
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amekagua na kuridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara ya Maji katika Mji wa Serikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
Aweso Akiwa eneo la ujenzi wa mradi amesema;
.
“Nitumie Nafasi hii kumshukuru Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia Fedha Zaidi ya Billioni 22.9 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hili na kupata mazingira mazuri kwa watumishi wetu wa Wizara ya Maji.”
Ujenzi huu wa jengo la Ofisi umefikia asilimia 96% ya ukamilifu wake huku likiwa na uwezo wa kuhudumia watu zaidi ya 518 ni jambo kubwa na lenye kuleta tija na ufanisi kwa watumishi wetu katika kutimiza majukumu yao.
Aidha,Aweso amewapongeza wataalamu toka Wizara ya Maji wanaosimamia ujenzi huu na Mkandarasi anayejenga Mradi huu na kusema kuwa kama Wizara wameridhika na kasi na viwango vya ujenzi wa jengo hilo.
.
Katika hatua nyingine Waziri Aweso amemuelekeza mkandarasi ahakikishe anakamilisha ujenzi huu kwa wakati na kwa mujibu wa mkataba.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

