Top news
TAEC YATAKIWA KUONGEZA JUHUDI YA UDHIBITI WA MIONZI
Serikali imesema inathamini kazi inayofanywa na Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) katika kudhibiti matumizi ya mionzi nchini na kuitaka taasisi hiyo kuongeza nguvu katika ukaguzi wa bidhaa zinazoingia nchini ili kuwalinda wananchi dhidi ya madhara ya mionzi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamata Shaame Khamis mara baada ya kutembelea maonesho ya NaneNane kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Peter Ngamilo amesema wanashiriki katika maonesho ya Nanenane ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya teknoliojia ya nyuklia huku mmoja wa waliofika katika banda ya TAEC akipongeza jitihada zinazofanyika.
.
Maonesho ya nanenane kitaifa mkoani Mbeya yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 08.08.2023 ambapo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sikukuu hiyo ya wakulima.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

