MSD YAANZISHA KIWANDA CHA MIPIRA YA MIKONO IDOFI MKOANI NJOMBE
Meneja Mipango, Ufuatiliaji Na Tathmini wa Bohari Ya Dawa (MSD) Bw.Hassan Ibrahim Amesema Katika kufanikisha ongezeko la uzalishaji wa bidhaa za afya nchini na kuendana na azma ya Serikali ya uanzishaji wa viwanda, MSD ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha miundombinu ya kiwanda cha mipira ya mikono kilichopo Idofi mkoani Njombe na kuanza uzalishaji ifikapo mwezi Septemba 2023.
.
Ibrahim Ameyasema hayo Leo Agosti 07,2023 Alipokuwa akizungumza Kwa niaba Ya Mkurugenzi Mtendaji Wa MSD Na Waandishi Wa Habari Kuhusu Utekelezaji Wa Majukumu ya Bohari Na Mwelekeo wake Kwa Mwaka Wa Fedha 2023/24 Katika Ukumbi Wa Idara Ya Habari Maelezo Jijini Dodoma.
.
Amesema Kiwanda hicho kitatoa ajira za moja kwa moja kwa watu takribani 200, Na Pia kitachagiza uzalishaji wa malighafi ya mpira hapa nchini na kupunguza utegemezi kutoka nje ambapo fedha za kigeni sawa na kiasi cha Shilingi bilioni 33 ambazo hutumika kila mwaka kuagiza mipira ya mikono nje ya nchi.
.
"Jukumu la uzalishaji litafanyika kupitia Kampuni Tanzu ya MSD iitwayo “MSD Medipharm Manufacturing Company Ltd” ili kuongeza ufanisi na kutoa fursa ya kushirikiana na sekta binafsi katika uzalishaji" Amesema Ibrahim.
.
Meneja Huyo Amesema Mikakati Yao Kwa Mwaka Wa Fedha 2023/24 Kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya na miundombinu ya utunzaji wake ambapo ujenzi wa maghala unatarajiwa kuanza mwezi Agosti 2023.
"Tutaanza uzalishaji wa mipira ya mikono kwa Kiwanda kilichopo kijiji cha Idofi, mkoa wa Njombe, Kujenga maghala ya kisasa katika mikoa ya Dodoma, Mtwara na Kagera kwa lengo la kuongeza nafasi za kuhifadhi bidhaa na kuimarisha ubora wa bidhaa za afya" Amesema.
.
Aidha, Ibrahim Amesema Kwa mwaka wa fedha 2022/23 Serikali kupitia MSD ilianza rasmi kutekeleza jukumu la usambazaji wa bidhaa za afya mara sita badala ya mara nne kwa mwaka. Usambazaji huu unaondoa tatizo la upatikanaji wa bidhaa za afya kwa kuhakikisha bidhaa zinafikishwa vituoni moja kwa moja kila baada ya miezi miwili.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

