logo

TCDC TUMESAJILI JUMLA YA VYAMA VYA USHIRIKA 7,300 MWAKA 2022/23

Mrajis wa Vyama Vya Ushirika Na Mtendaji Mkuu wa Tume Ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania(TCDC) Dkt.Benson Ndiege Amesema Kwa Mwaka 2022/2023 Tume imesajili jumla ya Vyama vya Ushirika 7,300, kati ya hivyo 77 ni Vyama vya Upili, 1 ni Shirikisho la Vyama vya Ushirika, 4,252 ni Vyama vya Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS), 2,034 ni Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) na 936 ni Vyama vinavyojishughulisha na kazi mbalimbali zikiwemo, ufugaji na uvuvi.

.

"Hadi kufikia Juni 2023, vyama vya Ushirika 5,424 kati 7,300 vimesajiliwa katika Mfumo wa Kidigitali wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) unaolenga kurahisisha usimamizi na uendeshaji wa Vyama vya Ushirika kwa nia ya kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji" Amesema.

.

Ndiege Ameyasema Hayo Alipokuwa Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Jijini Dodoma Kuhusu Utekelezaji Na Vipaumbele Vya Tume Hiyo Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24.

.

Amesema Mwelekeo Wa Tume hiyo Katika Kuimarisha Ushirika Kwa Mwaka 2023/2024 ni Kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika ili kuviwezesha Vyama vya Ushirika kupata Mikopo yenye Riba nafuu.

.

"Hadi kufikia Disemba 2024, Tume itakuwa imeshazindua Benki ya Taifa ya Ushirika (KCBL) na kuwa mali ya wanachama katika kujipatia mikopo ya kuendesha shughuli zao kikamilifu" Amesema Ndiege.

.

Mrajis Huyo Amesema Uwekezaji katika mifumo ya kisasa ya kidijitali itasaidia kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika Vyama vya Ushirika, pamoja na Mamlaka za Usimamizi.

.

Ndiege Amesema Hadi hivi Sasa Vyama vikuu vya Ushirika vimeajiri maafisa ugani 175 ambao wameendeleea kutoa huduma za ugani kwa wakulima katika mazao ya Tumbaku, Korosho, Pamba na Kahawa.

.

Aidha,Ndiege Amesema wamepanga Kufanya Uhamasishaji wa Uanzishwaji wa Vyama vya ushirika vya Mbogamboga katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe ambapo jumla ya wananchi 8,807 katika vikundi 222 na Vyama 18 vimesajiliwa.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn