logo

SIMBA SC BINGWA NGAO YA JAMII 2023

Simply Beautiful 🔥🫡 What a Match! What a drama🔥 Tumepata moja ya 'derby' bora kabisa kimbinu, kiuchezaji na kivipaji. Asante kwa wachezaji na walimu kwa mechi bora mno! Asante mwamuzi Jonesia! So good✅

Yanga SC wamekosa magoli tu mchezoni! Mpira waliocheza hauna shaka yoyote. Kila mtu anacheza kwenye njia na ni flow halisi ya mpira. Wakimpata mtu katili mbele ya goli wanaogofya.🔥🔥🫡

Kwa Simba ni kama Robertinho ukubwa wa kikosi unamchanganya. Hajui afanye nini! Uchaguzi wake wa kikosi cha kuanza na Sub zake ni mashaka matupu. Anapaswa kubadilika haraka mno vinginevyo watu hawatamvumilia.

Bakar Nondo na Ibrahim Bacca wana sanaa halisi ya ulinzi. Wakihitaji kubutua watafanya kwa usahihi, wakihitaji kucheza chini watafanya hivyo. Wanatoa 'basics' zote za ulinzi!

Mzamiru Yassin ni yule yule. Anatoa kila kitu kwa ajili ya timu na wenzie. Ni nani ana nishati kama yake pale Simba!? No. No. Kilomita nyingi uwanjani✅ Kupandisha timu✅

Unahitaji kiungo mwenye nidhamu na back four yake!? Nenda na Aucho! Mamlaka ya kiungo na usahihi wa pasi zake za kufanya mabadiliko kiuchezaji 'translation'. So Cool!

Che Malone Fondoh aliamua kuibeba shughuli very personal ✅ Ni bonge la beki na ilimchukua dakika chache kucheza na Kennedy Juma! Utulivu✅ Anticipation ✅

Attohoula Yao is all you need🙌✅ Kasi yake, krosi zake na uwezo wa kunusa hatari ni wa kiwango cha juu. Ana mapafu ya chui... Kila aliyeenda upande wake alionekana mzembe.

Respect Kennedy Juma! Ni ngumu kuamini kama huwa hachezi kila mara! Ameendana haraka na Malone.

So smart Maxi Nzengeli. Kwake mpira ni rahisi sana na masuala ya kugusana gusana sio muhimu.

ALLY SALIM ndiye Man of the Match🔥🫡! 5 stars performance! Ndio tendo gumu zaidi mpirani na aliye bora kisaikolojia hushinda. YANGA hawakufanya homework nzuri kuelekea kwenye penati! Wamepiga zote upande mmoja ambao ndio strength ya Ally✅

Wasalaam!

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn