
MBUNGE JANETH MAHAWANGA: KILA TAWI KATA YA WAZO LIWE NA MRADI WA KUJITENGENEZEA AJIRA
Mbunge Viti Maalum Wanawake Mkoa Wa Dar Es Salaam Mhe.Janeth Mahawanga Amewataka Wanawake wote kutoka Matawi 14 yanayounda Kata ya Wazo kuhakikisha kila Tawi linakuwa na mradi ili waweze kujitengenezea ajira miongoni mwao na kuondokana na utegemezi.
.
Vile vile Amewaomba Viongozi kuwa wabunifu hata kama ni wa ngazi ya Tawi kwani wana nafasi kubwa ya kuionyesha jamii kile walichonacho pamoja na kuwa wanaongoza ngazi ya Matawi.
.
Mahawanga Ameyasema Hayo Alipokuwa Kwenye uzinduzi wa mpango wa uanzishwaji Kiwanda cha ushonaji kama mradi wa Tawi la Kisanga Kata ya Wazo Tukio lililoenda Sambamba na kuwapokea Wanachama wapya wa UWT ambao wengi wao wanafurahishwa na kazi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
.
Kwa Upande mwingine, Mbunge Huyo Amewasisitiza Wanawake hao kuhakikisha wanaungana katika kutafuta maendeleo ya pamoja na kuwahakikishia kuwakutanisha kwenye vikao vyao na wadau muhimu wa maendeleo kama Sido, TBS, Kampuni za Bima, Taasisi za Kifedha, Brella, TIC, Maafisa Biashara wa Halmashauri na Wataalam wa Masoko ili kuwapa uelewa mpana wakati wakiendelea na taratibu za kukamilisha mradi huo.
.
Aidha, Mahawanga Amewataka Wanawake hao kuendeleza upendo na mshikamano katika safari ya kuelekea kwenye chaguzi zijazo lakini pia kugombea nafasi mbalimbali bila woga.
"niwahakikishieni Wanawake wa Tawi la Kisanga kuwa nipo nanyi bega kwa bega mpaka mradi wenu utakapokamilika kwani kiu yangu kubwa ni kuona maendeleo makubwa ya Wanawake ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam" Alisema Mbunge Huyo.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news