logo

NEEC YAWATAKA WAFANYABIASHARA KURASIMISHA BIASHARA ZAO ILI WAWEZE KUPATA MIKOPO,MAFUNZO NA FAIDA NYINGI

Katibu Mtendaji Baraza la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng'i Issa Ametoa Wito Kwa Wafanyabiashara wote Ambao Bado hawajarasimisha Biashara zao waweze Kufanya hivyo Kwani Urasimishaji unasaidia Mfanyabiashara aweze kupata Mikopo, Mafunzo Na Faida nyingi ambazo zinaendana na Urasimishaji.

.

"Ni Muhimu kurasimisha Biashara, Njia Ya Wewe Kuendelea Kupanda Juu Ni Kurasimisha Biashara Yako iwe Rasmi. ukifanya Hivyo utapata Mikopo, Mafunzo Na Faida nyingi Sana ambazo zinaendana na Urasimishaji" Amesema.

.

Beng'i Ameyasema Hayo Leo Agosti 14,2023 Alipokuwa akizungumza Na Waandishi Wa Habari Juu ya Mafanikio Katika Masuala ya Uwezeshaji Tanzania na Vipaumbele Vya Baraza Hilo Kwa Mwaka Wa Fedha 2023/24.

.

Amesema Kwa Mwaka Wa Fedha 2023/24 wamepanga Kuanzisha Mfumo Mzuri Wa Kidigitali Wa ukusanyaji Wa Taarifa na Kuweza Kuzichakata Taarifa Hizo na Kutoa Ripoti ya Kitaifa.

"Lakini vile vile tutakuwa Na Programu ya Kuongeza Ushiriki Wa Wanawake na Vijana Katika Manunuzi ya Umma" Amesema Beng'i.

.

Katibu Mtendaji Huyo Amesema Pia wamepanga kuunganisha Mifuko ya Uwezeshaji Ili iweze Kuleta Tija Katika Utoaji Wa Mikopo Na Dhamana Katika Benki za Biashara ambazo zipo hapa Nchini.

.

"Mchakato Huu ulishaanza Na Tunaendelea Kupata Maoni Ya Wadau, Lakini Tunategemea Mwaka Huu tutaifikisha Mwisho Kabisa"Amesema.

.

Aidha, Beng'i Amesema Mafanikio ya Baraza Hilo Kwa Kipindi Cha Mwaka Mmoja Uliopita Mifuko ya Uwezeshaji imetoa Jumla ya Mikopo Yenye thamani Ya Trilioni 6.1 Kwa wajasiriamali Milioni 8.6.

.

Naye Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Gerson Msigwa Amewataka Watanzania Kuwa makini, kujiridhisha kwanza kabla ya kuingia mikataba ya kuchukua mikopo ili kuepuka madhara yanayotokana na mikopo kutoka kwa taasisi zisizo rasmi.

"Mikopo yote inapitia kwenye ngazi za Halmashauri, fuateni taratibu zote ili kuepuka kutapeliwa hasa mikopo inayotangazwa mitandaoni" Amesema Msigwa.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn