logo

UGANDA YAKIRI WAFUGAJI KUCHANGANYA ARV KATIKA VYAKULA VYA MIFUGO

Maafisa kutoka Mamlaka ya Dawa Uganda (NDA) wamekiri kuficha taarifa kuhusu baadhi ya wakulima wanaochanganya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi na vyakula vya mifugo na kuku ili kukuza ukuaji wao.

NDA inadai kuwa wamekuwa wakifahamu kitendo hicho kwa zaidi ya miaka 10 lakini hawakuweza kuweka wazi taarifa hiyo ili kulinda uagizaji wa bidhaa nchini.

NDA wamekiri hayo baada ya kukutana na wabunge katika kamati ya bunge kuhusu VVU/UKIMWI.

"Wengi wetu tunakula mifugo hii bila kujua, sasa kuna madhara gani kwa kutumia dawa hizi".

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn