"TUNATAKA USHIRIKA UENDE KIDIJITALI NA KISASA ZAIDI" DKT.NDIEGE
Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt.Benson Ndiege amesema ni lazima vijana wapewe nafasi za ajira kwenye Vyama vya ushirika ili waweze kusimamia vizuri, kwa sababu vijana hao watakuwa na ndoto kubwa kuliko mtu ambaye ameshastaafu halafu akarudi kufanya kazi tena kwenye Vyama hivyo.
.
"Tunataka Ushirika uweze kwenda Kidijitali lakini uweze kwenda kisasa kuanzia kwenye Ajira mpaka kwenye usimamizi pia" amesema.
Ndiege ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao kazi kati ya Mrajis na Vyama Vya Ushirika vya Upili na Viongozi watendaji wa Vyama kilichofanyika leo Septemba 11,2023 katika Ukumbi wa Mabeyo Jijini Dodoma.
.
Amesema wameshafanya tathmini ya Vyama vikuu na kujua kila hali ya Chama kimoja kimoja na kinachotakiwa kama mtu aliajiriwa kwenye vyama hivyo na hana vigezo lakini sasa hivi Serikali na wadau wanasema lazima vigezo viwepo, hivyo kinachotakiwa vyama visimamie muongozo uliokuwepo.
.
Mrajis huyo amesema baadhi ya vyama vimekuwa vikipokea hati chafu kiutendaji suala hilo halikubaliki na tayari wameendelea kusisitiza, na pia wanachukua hatua kali kuhakikisha vyama hivyo havirudii makosa hayo.
.
"Mwaka Juzi tulifanya kikao cha Urafiki baada ya tatizo hilo kuwepo na kuonekana hali sio nzuri ya ripoti na tulipeana maelekezo kuna ambao walienda kufanya vizuri na mabadiliko yameonekana, Ripoti iliyopita ya mwaka jana 2022 bado ilikuwa na matatizo lakini ilikuwa bora kidogo kuliko iliyopita" amesema Ndiege.
.
Aidha, Dkt.Ndiege amesema mpaka hivi sasa bado hali haijatengamaa vizuri kwenye eneo hilo la hati chafu kama ambavyo kila mdau angependa kuona kwenye ushirika ikiwa mali zake zinatunzwa vizuri, taarifa zipo vizuri na wanapata hati ambazo ziko safi.
.
"kwahiyo ni uhalisia kuna mabadiliko Lakini bado hayatosha kuweza kuyasemea kwamba yamefika kiwango kizuri. ndio maana tunasema kila kikao na kila hatua tunayopita Lazima tulizungumzie Ili kuweka msisitizo" Amesema Ndiege.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

