logo

DKT.BITEKO AIPONGEZA BoT KWA UNUNUZI WA DHAHABU HAPA NCHINI

NAIBU Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania BoT kwa kununua dhahabu kwa ajili ya kutunza akiba za nchi badala ya kutunza kama fedha huku akisema ni ndoto ambayo Serikali ilikuwa inaitamani kwa muda mrefu.

Aidha ametoa wito kwa BOT kushirikiana kwa karibu na Wizara ya madini pamoja na taasisi zake ili waweze kumfikia kila mchimbaji kwa sababu kuna watu ambao hao wanaleta pesa wanakusanyiwa wanapelekewa dhahabu.

Akizungumza mkoani Geita katika maonesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini Mkoani Geita amesema kuwa kwa sasa nchi inahitaji fedha za kigeni kwa ajili ya manunuzi ambapo kwa upande wa dolla imekuwa changamoto kwa kila nchi duniani hivyo lazima zitumike rasimali za nchi katika kupata dolla na hawawezi kuipata bila kutumia dhahabu.

"Nia yetu ni kuona kwamba eneo linalotupatia fedha za kigeni kwa wingi bado itabaki kuwa sekta ya madini na sekta ya madini ikileta dolla kwa wingi hizo stress nyingine mnazoziona kama mafuta madawa na bidhaa zote tunazo ziagiza kutoka nje kwakutumia dolla tutaweza kuzipata ili tuhudumie watanzania kwa hiyo hongereni sana kwa hatua hiyo"amesema Biteko na kuongeza kuwa.

"Ni imani yangu baada ya miaka kadhaa nansisi kama nchi tuseme tuna akiba ya dhahabu tani kadhaaa kama ilivyo nchi nyingine kubwa na kuwapongeza wafanyazi wa BOT kwa hatua waliochukua ya ununuzi wa dhahabu."

Kwa upande wake Meneja Msaidizi Kurugenzi ya Masoko ya Fedha BOT,Dkt Anna Lyimo amesema kuwa mbali kununua dhahabu bado wanaangalia namna ya kuwasaidia wachimbaji wadogo na wa kati kutokana na changamoto zinazowakabili.

Ametaja baadhi ya changamoto hizo ni mitaji ,elimu na teknolojia ambapo wameamua kushirikiana na STAMICO ambao itasimamia wachimbaji hao kuungana kupitia vikundi ambapo BOT itawezesha kupata mikopo na kuondokana uchimbaji mdogo na kuinuka zaidi.

Ameongeza kuwa mbali zoezi la dhahabu pia wapo kwa ajili yakutoa elimu yakuhusina na sheria ya fedha za kigeni ya mwaka 2022 ambapo inataka matumizi ana mapato yote yanayopatikana katika mauzo ya nje ya nchi basi yaweze kurudishwa nchini ndani ya siku tisini na mapato hayo yanakuwa yanasaidia na kuongeza akiba za fedha za kigeni.

"Ninapenda kuishukuru Serikali kwakushirikiana bega kwa bega na BOT kuweza kufanikisha zoezi hili na tumeweza kulifanya kwa ufanisi na litakuwa na manufaa nakubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo "amesema Lyimo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn