logo

WACHIMBAJI WAASWA KUJILINDA DHIDI YA MAGONJWA YA MOYO

DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Salehe Mwinchete amewaasa wachimbaji kuchukua tahadhari dhidi ya kemikali wanazotumiankatika shughuli zao za uchimbaji màdini Ili kuepuka maradhi ya moyo yanayoweza kusababishwa na kemikali zinazotumika.

Hata hivyo Dkt.Mwinchete amesema hakuna madhara ya Moja kwa Moja ya moyo yanayoweza kusababishwa na kemikali zinazotumika katika uchimbaji wa Madini.

Dkt.Mwinchete ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi katika kliniki ndogo ya magonjwa ya moyo iliyopo katika eneo la.maonesho ya madini katika kata ya Bombambili katika halmashauri ya mji wa Geita mkoani Geita.

"Naweza kuwahakikishia kwamba kemikali mbalimbali zinazotumika katika uchimbaji na kuandaa madini hazina madhara ya Moja kwa Moja isipokuwa wachimbaji na wahusika wote katika sekta ya madini wanatakiwa kuchukua tahadhari kuhakikisha kwamba wanazingatia kemikali ambazo zinaweza kuleta athari katika mwili wa binadamu zinazoweza kuleta athari katika moyo japokuwa siyo athari za Moja kwa.moja kwenye moyo."amesema na kuongeza kuwa

"Lakini watu wanaochimba madini ni kama watu wengine kwamba watakuwa katika athari ya kuugua ugonjwa moyo kama hawatazingatia habari ya mazoezi,unywaji pombe kupitiliza na uvutaji wa sigara ni athari kwa Afya zao lakini pia kuzingatia namna na aina ya vyakula wanavyotumia."

Amewataka wananchi Kujenga utaratibu wa kupima Afya zao mara kwa mara Ili tatizo lionelane mapema na kupatiwa Tiba huku kwa ambao hawajapata maradhi waweze kushauriwa na kuendelea kuwa salama.

DKt.Mwinchete amesema JKCI imeleta kliniki ya maalum"V.I.P" ya huduma ya magonjwa ya moyo,Kliniki hiyo maalum inapatikana katika maonyesho ya sita(6) ya madini yanayofanyika kuanzia tarehe 20 september mpaka 30 September mwaka katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

Aidha,Dkt Salehe amefafanua jinsi kliniki hiyo inavyotoa huduma alisema "Mtu ataomba siku na muda ambayo anataka kuja kuhudumiwa katika kliniki maalum, atukutana na mazingira mazuri ya huduma,atafanyiwa huduma zote hapo hapo alipo kwa maana atamuona daktari hapo hapo,atapata vipimo hapo hapo na pia atapatiwa kiburudisho cha chai akiwa anasubiria majibu

Pia Dkt Salehe ameelezea vyanzo tofauti tofauti vya maradhi ya moyo alisema kuwa ni ulevi,uvutaji wa sigara,matumizi ya chumvi nyingi katika chakula hivyo ameitaka na kuhihasa jamii kupunguza matumizi ya sigara na pombe ili kuepukana na maradhi ya moyo.

Aidha,Dkt Salehe amefafanua jinsi kliniki hiyo inavyotoa huduma alisema "Mtu ataomba siku na muda ambayo anataka kuja kuhudumiwa katika kliniki maalum, atukutana na mazingira mazuri ya huduma,atafanyiwa huduma zote hapo hapo alipo kwa maana atamuona daktari hapo hapo,atapata vipimo hapo hapo na pia atapatiwa kiburudisho cha chai akiwa anasubiria majibu"

Pia Dkt Salehe ameelezea vyanzo tofauti tofauti vya maradhi ya moyo alisema kuwa ni ulevi,uvutaji wa sigara,matumizi ya chumvi nyingi katika chakula hivyo ameitaka na kuhihasa jamii kupunguza matumizi ya sigara na pombe ili kuepukana na maradhi ya moyo.

Pamoja na majukumu makubwa ya Taasisi ya Jakaya Kikwete Kwa matatizo ya moyo tunaelimisha, na kujenga uwezo kwa Wataalam mbalimbali kwa maradhi ya moyo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn