logo

MSALABS YAWEKEZA TSH.BILIONI 5 MAABARA UPIMAJI WA MADINI

MAABARA ya upimaji wa sampuli za Madini (MSALABS) yenye Makao Makuu yake nchini Canada , imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 5 za kitanzania kwa ajili ya upimaji wa sampuli hizo kwa kiwango cha Kimataifa.

.

Mkurugenzi Mtendaji wa Maabara hiyo Mugisha Lwekoramu amesema hayo Septemba 27, 2023 Mbele ya Waziri wa Madini Anthony Mavunde wakati wa uwekeji wa jiwe la msingi wa maabara hiyo iliyojengwa katika halmashauri ya Mji wa Geita mkoani Geita.

.

Lwekoramu amesema Maabara hiyo inatumia teknolojia ya kisasa ya upimaji wa sampuli kwa kutumia mionzi ambayo pia husaidia katika utunzaji wa mazingira tofauti na teknolojia ya awali ya kutumia kemikali na moto lakini pia hutoa majibu kwa muda mfupi.

.

Maabara hii inatumia teknolojia ya kisasa ya upimaji wa madini kwa mionzi ambayo ni rafiki hata kwa mazingira yetu maana haitumii kemikali wala moto katika upimaji na hutoa majibu ya ufanisi mkubwa.

.

“Pia Teknolojia humwezesha mteja kupata ,majibu ya sampuli ndani ya muda mfupi sana ukilinganisha teknolojia za zamani za kutumia moto na kemikali ambazo majibu huchukua siku kadhaa ikiwemo uwezekano wa kuwa na makossa ya kibinadamu na mwisho wa upimaji sampuli huwa imeharibika kabisa,kwa hiyo teknolohjia hii ya kisasa baada ya upimaji kukamilika mteja ana uhuru wa kuondoka na sampuli iliyo katika ubora wake wa awali .”amesema Lwekoramu.

.

Aidha, amesema kwa asilimia 99.8 ya wafanyakazi wa maabara hiyo ni watanzania ambapo matarajio yao ni watanzania hao kujifunza teknolojia hiyo ya kisasa ili waweze kueneza ujuzi wa teknolojia hiyo hapa nchini kwa kadri teknolojia jiyo itakavyoendelea kukua.

.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Martine Shigela amesema uwekezaji huo ni kutokana na ukweli uliopo kwamba nchi ina Rais anayesimamia na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn