logo

WATUMISHI DUWASA WATAKIWA KUHUDUMIA WATEJA KWA SPIDI YA 6G

KATIKA kusheherekea Wiki ya Huduma kwa Mteja ambayo imeanza leo Oktoba 2, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph amewataka watumishi wa Mamlaka hiyo kuhudumia wateja kutoka kwenye spidi ya 3G kuhamia 6G.

Amesema kama hawawezi kuwahudumia wateja ipasavyo basi hakuna maana ya kuwa katika nafasi hizo.

“Lazima tujiweke katika mazingira ya kuwapendezesha wateja wetu, mteja akija amepanda wewe shuka msikilize, mteja siku zote anahaki na sisi tuna wajibu wa kumsikiliza.” Amesema Mhandisi Aron.

Amesema kuna wengine hawawezi kujieleza na utakuta mteja anashida muhimu, ni wajibu wako wewe kumsikiliza na kumuelewa na kumsaidia.

Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa Mteja yenye kauli mbiu 'Huduma ya Maji kwa Pamoja' DUWASA imetembelea gereza la Isanga na kutoa msaada, na inatarajia kutembelea wateja wakubwa na wadogo na pia kutembelea wateja mtaani na maeneo ya Soko la Machinga, Sabasaba na Majengo ili kuzungumza na wateja wa Mamlaka.

@duwasatz

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn