WAZAZI,WALEZI WATAKIWA KURUDI KWENYE MALEZI YA WATOTO WAO
Utekelezaji wa Mpango wa Malezi na Makuzi kwenye vituo vya kijamii (ECD Centers) vinavyokwenda kujengwa nchi nzima, utawanufaisha wazazi kwa kuwapatia elimu kuhusu malezi ya watoto.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt.Dorothy Gwajima, akifungua mafunzo ya wakufunzi wa watoa huduma ya malezi kwa watoto, mkoani Morogoro Oktoba 02, 2023.
Waziri Dkt.Gwajima amewaasa wazazi na walezi kurudi kwenye wajibu wao wa malezi ya watoto ili watakapokua, wawe wameshika maadili.
“Asilimia 53 ya watoto Tanzania, haiko kwenye mfumo mzuri wa kuweza kupata yale wanayotakiwa kuyapata kama watoto ili wakue vizuri, hapa nazungumzia changamoto za mmomonyoko wa maadili, afya, lishe na elimu,” amesema Gwajima.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Sebastian Kitiku, amesema kuna changamoto ya wazazi kuwa na msongo wa mawazo unaopelekea kuwa na changamoto za afya ya akili zinazowasukuma kuwafanyia ukatili watoto wao, hivyo programu ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto itasaidia kutimiza malengo ya Serikali.
Mafunzo hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum pamoja na Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani(UNICEF) kwa kuwaleta pamoja wataalamu kutoka Serikalini na Sekta Binafsi.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

