logo

TAKUKURU NA DCEA WAZINDUA KAMPENI YA 'TOKOMEZA RUSHWA NA DAWA ZA KULEVYA SHULENI NA VYUONI'

Wito umetolewa kwa jamii kutoa ushirikiano kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) na Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Ili kufanikisha Kampeni ya "TOKOMEZA RUSHWA NA DAWA ZA KULEVYA, SHULENI NA VYUONI" ili kujenga Tanzania isiyokuwa na Rushwa wala Madawa ya Kulevya.

.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)CP Salum R.Hamduni Leo Oktoba 04,2023 alipokuwa wakizindua Kampeni hiyo pamoja na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA)CG Aretas J.Lyimo tukio lililofanyika Jijini Dodoma.

.

Amesema matarajio yao kampeni hiyo ikitekelezwa kwa ushirikiano na wadau wote nchini ikiwemo waandishi wa habari na wadau wote hususani katika ngazi ya elimu itachangia kuongeza uelewa kwa wanafunzi,vijana na jamii kwa ujumla kuhusu ukubwa wa tatizo la Rushwa na madhira ya madawa ya kulevya.

.

"Tunasema Madhira ya Dawa za kulevya kwa Sababu Vitendo Vya Rushwa na Biashara Pamoja na Matumizi ya Dawa za kulevya zina madhara makubwa Kiuchumi,kijamii na kisiasa.

.

"Vitendo hivi vinarudisha nyuma nguvu kazi ya Taifa kwa kusababisha ulemavu,Vifo,kuwa na walaigbu wengi wa dawa za kulevya, gharama kwa serikali katika kuwahudumia pamoja na kupoteza mapato ya Serikali" amesema CP Hamduni.

.

Kwa Upande wake Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA)CG Aretas J.Lyimo amesema lengo kuu la Kampeni hiyo ni kuelimisha Umma kuhusu tatizo la Dawa za kulevya na mahusiano ya ushiriki na kukabiliana na matatizo

hayo Ikiwemo rushwa pamoja na Dawa za kulevya.

.

"Matarajio ya Kampeni hii Kuwa yatawajengea Uwezo wanafunzi, Wanachama wa klabu za wapinga rushwa na wananchi Kwa Ujumla juu ya Uelewa Wa Tatizo la Rushwa na uhusiano wake na dawa za kulevya.

.

"Hapa tutapata uhusiano Wa Rushwa na Madawa ya Kulevya,hivyo wanafunzi wale tunaowafundisha Vyuoni watakuwa na Huo uelewa Wa Rushwa na madhara yake na pia hivyo hivyo Kwa madawa ya kulevya hapo tutajenga Taifa Bora" amesema Kamishna Jenerali huyo.

Aidha, CG Lyimo amesema kupitia Taasisi hizo Mbili (TAKUKURU na DCEA) wanakwenda kuhakikisha Tanzania inakuwa kiuchumi na pia wanajenga taifa la watu Wenye Uadilifu.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn