logo

WAZIRI MKENDA: SEKTA BINAFSI KWENYE ELIMU SIO MSHINDANI WA SERIKALI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema sekta binafsi kwenye elimu sio mshindani wa Serikali,bali sekta binafsi kwenye elimu ni mshirika wa serikali hivyo watafanya kazi na wamiliki wa shule zisizo za serikali kwa mtizamo huo na pia wataangalia uwezekano wa kwenda hatua moja mbele zaidi.

.

Prof.Mkenda ameyasema hayo Oktoba 10,2023 alipokuwa akihitimisha Mkutano wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wamiliki wa Shule zisizo za Serikali nchini tukio lililofanyika Jijini Dodoma.

.

Mkenda aliahidi ya kwamba watakwenda kuchambua kila kitu iwezekanavyo na kuhakikisha kwamba wanatekeleza yale ambayo yanawezekana.

.

Waziri huyo pia alisema wataangalia uwezekano wa kuitekeleza program ya PPP na wamiliki hao hasa katika utoaji wa mafunzo ya amali ni mapema sana Ili kuweza kuongeza kasi ya utoaji mafunzo hayo.

.

"Hiyo ni kuonesha kwamba tunathamini sana sekta binafsi na tumaini langu tutapata mkakati mzuri wa kutekeleza hilo" Alisema Mkenda.

.

Mkenda alisema ubaguzi dhidi ya shule binafsi sio sahihi,hautakiwi kabisa hivyo watajaribu kuhamasishana ndani ya serikali Ili kuhakikisha kwamba wakati wa kujaribu kutoa huduma kwa umma kipaumbele ni sehemu ambazo zina taasisi,kampuni ya uzalishaji, kuna hospitali, Shule nk. bila kujali ni ya umma au ni binafsi.

.

Aidha, Mkenda alisema katika mageuzi ya mitaala wanahitaji sekta binafsi iende sambamba na wao hivyo upande wa maandalizi ya walimu watahangaika kadri vile inavyowezekana ili waweze kufanya pamoja na wamiliki hao.

.

"Kila inapowezekana tufanya kila kitu Bila kutoza Chochote ili kuhakikisha walimu wanakuwa tayari kwa ajili ya mabadiliko ya mitaala" alisema Mkenda.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn