TAX: TUNAENDELEA KUWARUDISHA WATANZANIA KUTOKA SUDAN
SERIKALI ya Tanzania imeendelea na jitihada za kuwarejesha Watanzania kutoka Jamhuri ya Sudan kufuatia mapigano yanayoendelea nchini humo kati ya kikosi cha Jeshi la Sudan na kikosi cha Msaada wa Jeshi yaliyoanza tarehe 15 Aprili, 2023.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.Stergomena Tax (Mb) amesema kuwa zoezi la kuwarejesha watanzania waliopo nchini Sudan si jepesi kwani viwanja vya ndege hususan Khartoum ambako ndiko kwenye mapigano vimefungwa.
Kufuatia siku tatu zilizotolewa za kusitisha mapigano (kati ya tarehe 21 23 Aprili 2023) tumeweza kuwasafirisha watanzania 200 (wanafunzi, watumishi wa Ubalozi, na raia wengine) kupitia mpaka wa Matema, Ethiopia kwa magari na wote wapo salama, alisema Dkt. Tax
Tax ameongeza kuwa Watanzania hao watasafirishwa kwa ndege ya Shirika la ndege la ATCL kuja Tanzania. Ndege hiyo ipo tayari kuwachukuwa na kuwarejesha nyumbani.
Kwa upande mwingine, Tax amemshukuru kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuongoza zoezi hilo kwa ujasiri na bila kuchoka, hadi kufanikisha kufikia hatua hii.
Aidha, Waziri Huyo amezishukuru taasisi zilizoshirikiana na Wizara kwa kujituma na kufanikisha zoezi hilo. Taasisi hizo ni pamoja na; Ofisi ya Rais, Balozi za Tanzania nchini Sudan, Ethiopia na Misri na pia Shirika la ndege la ATCL.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

