logo

MAGUGU MAJI YAVAMIA ZIWA BABATI MKOANI MANYARA

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga(@queen__sendiga) amemuomba Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Suleimani Jafo kuongezwa nguvu zaidi ya Kifedha kutoka wizarani ili kupata teknolojia sahihi zaidi itakayosaidia kuharakisha zoezi la kulinusuru ziwa Babati ambalo limevamiwa na magugu maji

Sendiga ameyasema hayo Novemba 14,2023 mkoani humo mara baada ya kupata ugeni wa Waziri huyo ambapo alipata nafasi ya kumpitisha na kutazama uvamizi wa magugu maji katika ziwa Babati.

Mkuu huyo alimuonyesha Mhe.Waziri kasi ya uvamizi huo na kuonyesha jitihada zinazoendelea za kuondoa magugu maji kwa kutumia mikono ambazo huenda zikagonga mwamba kufuatia magugu maji kufikia maeneo ya kina kirefu cha ziwa.

Aidha,Mhe.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Suleimani Jafo, alilipokea ombi lao na kuahidi kulifanyia kazi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn