logo

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAPOKEA MAGARI 2 KUTOKA UK-AID

Wizara ya Elimu ya, Sayansi na Teknolojia imepokea magari 2 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 250 kutoka kwa Shirika la maendeleo la Uingereza la UK-AID kwa ajili ya ufuatiliaji na tathimini ya shughuli za kielemu za program za Shule Bora nchini.

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika leo Novemba 16,2023 katika Ofisi za Taasisi ya Elimu Tanzania Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt.Franklin Rwezimula amepokea magari hayo na kuyakabidhi kwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt.Charles Msonde tayari kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula amelishukuru Shirika la maendeleo la Uingereza la UK-AID kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita katika kuboresha Sekta ya Elimu kwa kutoa magari hayo yatayosaidia utekelezaji wa mradi huo.

“Tunashukuru kwa msaada huu, kwani utaimarisha ufuatiliaji na tathmini katika miradi ya elimu ambao umekuja wakati muafaka ambapo Serikali inaweka mkazo katika kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kubaini changamoto mbalimbali”.Amesema Rwezimula.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Dkt.Charles Msonde amesema kuwa,TAMISEMI kama watendaji katika ngazi za mikoa na Serikali za Mitaa wataendelea kutoa ushirikiano kwa mashirika yanaoendelea kusaidia katika kuboresha masuala mbalimbali ikiwemo elimu nchini.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo wa Ubalozi wa Uingereza hapa nchini, Bi.Kemi Williams ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano walionesha katika kuhakisha magari hayo yananuliwa ili kwenda kusaidia katika mradi wa shule Bora utaosaidia maboresho katika Sekta ya elimu nchini kupitia ufuatiliaji na tathmini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TET,Dkt.Aneth Komba amesema TET kama watekelezaji wa mradi wa Shule bora kupitia mafunzo tayari,imetoa mafunzo kwa walimu na viongozi mbalimbali wa elimu nchini yakiwemo ya mbinu za ufundishaji na ujifunzaji zinazozingatia ujumuishi wa walimu.

Progamu ya Shule Bora inatakelezwa katika mikoa 9 ya Tanzania Bara ambazo zina halmashauri 67.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn