MBUNGE SALIM ALMAS ATOA MIL 13 KWAAJILI YA LESENI ZA WACHIMBAJI WADOGO KATA YA LUKANDE.
#Repost @jordanmedia_
Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe.Salim Alaudin Hasham ametoa kiasi cha Milioni kumi na tatu (13,000,000) kwa ajili ya malipo ya leseni za wachimbaji wadogo wanaofanya kazi zao za uchimbaji wa madini katika kata ya Lukande wilayani humo.
Hatua hiyo imekuja baada ya wachimbaji hao kulalamika kwa mbunge kuwa wanashindwa kufanya shughuli zao za uchimbaji kutokana na kushindwa kulipa fedha ya leseni jambo lililopelekea kuzuiwa kufanya shughuli hizo katika maeneo hayo huku wao wakitegemea kazi hiyo kwaajili ya utafutaji wa riziki zao.
Akiwasilisha kero hiyo kwa niaba ya wachimbaji hao Diwani wa kata hiyo ya Lukande, Novatus Majiji amesema wachimbaji wanamchango mkubwa sana katika kata hiyo hivyo kwazuio hilo la kuacha uchimbaji kutokana na kukosa fedha ya leseni itasababisha vijana wengi kushindwa kuendesha maisha yao.
Akizungumza katika mkutano wake na wananchi Mbunge wa Jimbo hilo la Ulanga Mhe.Salim Alaudin Hasham amesema yeye binafsi atawalipia kiasi hicho cha fedha ili waendelee na shughuli zao na amewataka kuwa makini pindi wanapopata madini wakumbuke kulipia leseni zao ili kuondokana na changamoto ya zuio hilo kwa wakati mwengine kutokana na deni la leseni.
Kata ya Lukande inazaidi ya wachimbaji wadogo wadogo 300 ambao wanachimba madini ya vito katika kata hiyo.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

