KIHARUSI HATARI KWA NCHI ZINAZOENDELEA, BENJAMIN MKAPA HOSP MATIBABU YANAPATIKANA
Tafiti zinaonesha kuwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zinakabiliwa na wimbi la ongezeko la wagonjwa wa kiharusi, ugonjwa huo ukichangia vifo mara tatu zaidi kulinganisha na nchi zilizoendelea.
Tafiti za kisayansi ukiwemo wa Dkt. Sarah Matuja “the rising tide of stoke in Tanzania: an argent call for action” zinaweka wazi kuwa asilimia 45 ya visa vya kiharusi vingeweza kuepukika kwa kupima shinikizo la juu la damu na kulidhibiti.Dkt.George Dillunga, ni Bingwa wa Magonjwa ya Dharura na Mkuu wa Idara hiyo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma, anafafanua hatua kwa hatua kuhusu KIHARUSI.
“Ziko aina nyingi za kiharusi” anaanza kwa kusema Dkt.Dilunga, na kisha kutaja dharura hizo kuwa ni “Kiharusi kinachotokana na mishipa ya damu kupasuka na Kiharusi kinachotokana na mishipa ya damu kuziba”
Kiharusi cha aina ya kwanza kinachotokana na mishipa ya damu kupasuka husababishwa na kupasuka mishipa ya damu ndani ya ubongo huku kinachotokana na mishipa kuziba mara nyingi husababishwa na damu kuganda.
Shirika la Afya Duniani WHO, linaweka wazi kuwa watu milioni 15 hukabiliwa kiharusi kila mwaka, kati yao watu milioni 5 hupoteza Maisha huku Milioni 5 wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu.
Kwa mujibu wa Dkt.Dilunga, ikiwa wagonjwa wa KIHARUSI watapatiwa dharura ya matibabu kwa haraka kukabili changamoto kinazoleta mwilini itaepusha wagonjwa kupatwa na madhara mengi na kuepusha vifo.
“Shinikizo la damu, Kisukari, Uvutaji sigara, Tatizo la moyo hasa mapigo ya moyo tofauti, Kiharusi kilichopita au Kiharusi kidogo cha Muda (TIA), Umri na Historia ya Familia ni baadhi viashiria vya uwezekano wa kukabiliwa na KIHARUSI” Alisema Dkt. Dilunga.
Watu wenye kiharusi wanaweza kuwa katika hali ya Kupooza ghafla au udhaifu kwenye uso, mkono, au mguu Kushangaa Matatizo ya kusema au kuelewa Maumivu makali ya kichwa bila sababu inayojulikana.
@bmhdodoma
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

