logo

NMB YAGAWA MIZINGA 500 MIKOA YA MOROGORO, TABORA NA NJOMBE

Benki ya NMB(@nmbtanzania) Leo Novemba 20,2023 imezindua programu yao ya ugawaji Mizinga ya Nyuki yenye manufaa kwa jamii hasa katika juhudi za kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, wakishirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

NMB wameanza na mizinga 500 kwa Mikoa mitatu ya Morogoro, Tabora na Njombe huku wakilenga Kusaidia jamii zilizozungukwa na rasilimali misitu na wanyamapori, kujipatia kipato mbadala ili kupunguza utegemezi wa kipato unaotokana na uvunaji ovyo wa misitu kwenye maeneo ya hifadhi, Kuimarisha ulinzi wa makazi ya Nyuki kwani wanasaidia uwepo wa chakula kwa sababu nyuki huchambusha mbegu ambazo baadae huzaa matunda ambayo hutumika kama chakula cha binadamu na wanyama.

Na pia Kufikia vikundi 17 katika mikoa mitatu ambapo zaidi ya wanavikundi 300 watapata elimu ya utunzaji wa mazingira, pamoja na kupata njia bora ya kisasa ya uvunaji wa asali.

Aidha,Mradi huo ambao pia utatoa elimu ya ujasiriamali na kifedha kupitia Taasisi yao ya NMB Foundation, umezinduliwa mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Hassan Abbas aliyeambatana na viongozi wengine wa serikali, huku wakiwakilishwa na Afisa Mkuu wao wa Wateja Wakubwa na Serikali- Alfred Shao.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn