BENKI YA NMB KINARA WA TUZO 2023 TANZANIA
Jana tarehe 24 Novemba 2023 kwenye siku ya Mlipa Kodi 2023, Benki ya NMB(@nmbtanzania) iliibuka mshindi wa jumla kitaifa, kama mlipa kodi mkubwa zaidi Tanzania na kama mlipa kodi bora zaidi anayelipa kodi kwa hiari (Most Compliant Tax Payer).
Huu unakuwa ni mwaka wa pili mfululizo kwa Benki ya NMB kupata tuzo hizo.
Jumla ya tuzo walizozipata Benki ya NMB ni Mshindi wa Jumla Kitaifa: Taasisi inayolipa Kodi kubwa zaidi nchini Tanzania (Sekta zote), Mshindi wa Jumla Kitaifa: Taasisi Bora inayolipa kodi kwa hiari kwa kuzingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi (Most Compliant Tax Payer).
Na pia mshindi wa Kwanza: Mlipa Kodi mkubwa zaidi katika kundi la Taasisi za Fedha nchini Tanzania (mara ya tatu mfululizo).
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi.Ruth Zaipuna alisema tuzo hizo ni matokeo chanya ya misingi imara ya utawala bora na uadilifu, kuzingatia kanuni za ulipaji kodi, ufanisi katika kuendesha biashara na ubunifu wa suluhishi bora za kifedha kwa wateja.
“Nawashukuru wateja wetu na Watanzania wote kwa kuendelea kuiamini Benki ya NMB kama mshirika wao kwenye biashara na shughuli zao, naishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufanya Biashara nchini na kipekee nawashukuru wafanyakazi wenzangu wote wa Benki ya NMB kwa kuendelea kufanya kazi kwa ari, bidii na kwa uzalendo mkubwa kwa maslahi mapana ya Benki na nchi yetu kwa ujumla.” alisema Zaipuna.
Tuzo hizo za Mamlaka ya Mapato Tanzania zimetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Dotto Biteko katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Aidha,Kama mdau wa maendeleo, Benki ya NMB imesema itaendelea kuendesha biashara yao kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuendelea kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa Taifa letu.
@nmbtanzania
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

