logo

KOCHA TERRY VENABLES AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 80

Kocha wa zamani wa England, Tottenham na Barcelona Terry Venables amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80, familia yake imethibitisha kutokea kwa kifo chake.

Venables aliiongoza England kutinga nusu fainali ya Euro 96 kwenye ardhi ya nyumbani.

Akiwa meneja wa klabu, aliiongoza Tottenham kutwaa Kombe la FA mwaka wa 1991 na kushinda La Liga na Barcelona mwaka wa 1985.

.

Pia alisimamia Crystal Palace,QPR, Middlesbrough na Leeds United wakati wa ukocha uliochukua miongo minne.

Taarifa iliyotolewa kwa Chama cha Wasimamizi wa Ligi kwa niaba ya familia ya Venables ilisema:

"Tumesikitishwa sana na kufiwa na mume na baba mzuri ambaye aliaga dunia kwa amani jana baada ya kuugua kwa muda mrefu.

"Tungeomba faragha itolewe wakati huu wa kusikitisha sana."

Klabu imesikitishwa sana na taarifa ya kifo cha mchezaji wa zamani huyo.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn