logo

PROF.NUNGU:TUWAUNGE MKONO,TUWAPE NAFASI WABUNIFU

MKURUGENZI Mkuu Wa Tume Ya Taifa Ya Sayansi Na Teknolojia (COSTECH) Dkt.Amos Nungu Ametoa wito Kwa Wananchi Na Wadau Kwa Ujumla kuthamini Na Kuwapa Nafasi Wabunifu Wa Vitu Mbalimbali Hapa Nchini Ili waweze Kuonekana Na Kukuza Ubunifu Wao Katika Taifa Letu.

.

"Wabunifu Tuwaunge Mkono, Tuwape Mrejesho Kupitia Ubunifu Wao Ili waweze Kuboresha"

.

Nungu Ameyasema Hayo Leo April 27,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Katika Maonesho Ya Wiki Ya Ubunifu yaliyofanyika Katika Uwanja Wa Jamhuri.

.

Nungu Amesema Mwaka Huu 2023 Watu waliokuja Kuonyesha Vitu Vyao Katika Wiki Ya Ubunifu ni Wengi Zaidi Kutoka Kada Mbalimbali huku Ubunifu ukiwa wenye Viwango Mbalimbali.

.

"Tuna Wenzetu Kutoka Africa Kusini Ambao Ni COSTECH YA Afrika Kusini Kwenye Masuala ya Ubunifu, wamekuja Ili kuonesha Thamani ya Kwamba hili Tukio linazidi Kwenda Kimataifa.

.

"Afrika Kusini Huwa Tunashirikiana Nao Katika Kujifunza mambo Mbalimbali Kutoka Kwao Na Hata Kutoka Kwetu, Na Kuna Nyakati Tulishawahi Kufadhili Kwa Pamoja ambazo zilikuwa Ni Bunifu Tatu na Vijana Wakaja Na Ubunifu" Amesema Nungu.

.

Aidha, Mkurugenzi Huyo Amesema Wanaamini Mwakani 2024 yatakuwa Maonesho mazuri Zaidi Kushinda ya Mwaka Huu 2023 Kutokana Na Walivyojipanga Kwenye Maandalizi ya Tukio Hilo.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn