logo

HUDUMA YA MTOTO NJITI NI YA UHAKIKA SASA KIGAMBONI

Mkuu wa wilaya Kigamboni Mhe.Halima Bulembo ameipongeza Taasisi ya Doris Mollel kwa vifaa tiba walivyomkabidhi leo katika hospitali ya wilaya kigamboni ambavyo vinaenda kuanzisha wodi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

"Tumefuta kauli ya hakuna vifaa, kwasasa hatutakua na rufaa tumeletewa msaada huu wenye thamani kubwa turudishe dhumuni la wasamaria wema waliochangia kupitia Taasisi ya Doris Mollel.kwa sasa tukizungumzia watoto njiti tunajivunia kazi nzuri mnayoifanya".

Bulembo ameyasema hayo leo Novemba 29,2023 katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 30 katika hospitali ya wilaya Kigamboni jijini Dar Es Salaam.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Dkt.Lucas Davis Ngawitu amesema watoto njiti 54 wamezaliwa kutoka mwezi Januari mpaka sasa na hao wote walipewa rufaa kwenda Temeke.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn