DKT.MASHIMBA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI NA UTUNZAJI MAZINGIRA CHAMWINO, DODOMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Dkt.Semistatus Mashimba ametoa wito kwa wanafunzi katika shule mbalimbali nchini na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanadumisha suala la utunzaji mazingira na upandaji wa miti ili kuepusha ukosefu wa mvua na kuondokana na hali ya jangwa.
.
Dkt.Mashimba ameyasema hayo leo Novemba 30,2023 alipokuwa akizindua kampeni ya upandaji miti na utunzaji wa mazingira, na uzinduzi wa mashine ya kuchakata mkaa mbadala ili kutunza mazingira na kutokata miti ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika shule MAMA wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
.
Amesema kila mzazi anapaswa kuhakikisha anapanda miti hata katika maeneo ya makazi yao, na kama maji ni changamoto basi wapande miti hata kwenye visado.
.
"Suala la kupanda maua,miti ndio malengo ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan. Kila mara kila muda amekuwa akitusisitiza kuhusu masuala ya mazingira tuhakikishe tunatunza na kupanda miti yetu" alisema Mashimba.
.
Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema unapozungumzia miti ya matunda ni mchango mkubwa wa taifa hili kwenye masuala ya lishe, hivyo katika shule zote miti ya vivuli na matunda ikipandwa watoto watapata lishe kupitia matunda.
.
Aidha, Dkt.Mashimba amelipongeza Shirika la Equality for Growth kwa kuleta programu hiyo ya mazingira kwa wanafunzi shuleni ni jambo la muhimu sana.
Kwa upande wake Afisa mazingira wa halmashauri ya Chamwino Bi.Yustina Ano amesema katika program hiyo mpaka sasa hivi wamefanikiwa kupanda miti 30 katika eneo la shule hiyo, ambapo ilikuwa ni miti ya matunda ya aina mbalimbali na miche 8 ilioteshwa katika eneo la serikali ya kijiji.
"Kwahiyo leo tutakwenda kupanda miti iliyoasiwa 20 hapa hapa katika eneo la shule, kwenye kitalu tumeotesha Miche 70. mradi ni mdogo na ni hatua ya mwanzo, na ninaamini kadri tunavyoendelea tutafikia maeneo mengi zaidi" alisema.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

