logo

MARUFUKU KUMNYANYAPAA NA KUMBAGUA MTU MWENYE VIRUSI VYA UKIMWI- WAZIRI MKUU MAJALIWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amesema kiwango cha ushamiri wa VVU kwa umri kuanzia miaka 15 na zaidi kwa mikoa ya Tanzania bara kinaanzia asilimia 1.7 kwa Mkoa wa Kigoma hadi kufikia asilimia 12.7 kwa Mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa.

.

"Mkoa wa Njombe una viwango vya ushamiri zaidi ya asilimia 9 sawa na mara mbili ya kiwango cha Taifa"

Mhe.Majaliwa ameyasema hayo leo Disemba 01, 2023 alipokuwa mkoani Morogoro akihutubia katika maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo Kitaifa yamefanyika mkoani humo.

Amesema maambukizi mapya miongoni mwa watu wazima zaidi ya miaka 15 yanaendelea kupungua kutoka watu 72,000 waliokuwepo mwaka 2016/2017 hadi watu 60,000 kwa mwaka 2022/2023. Hii ni sawa upungufu wa asilimia 0.18.

"Tanzania imepiga hatua kubwa na imepata mafanikio mazuri katika kufikia malengo ya 95-95-95 ifikapo mwaka 2025.

"Ninawapongeza sana wadau wote na wananchi kwa ujumla kwa ushirikiano uliowezesha kufikiwa hatua hiyo" amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali haitosita kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya unyanyapaa na ubaguzi kwa wenye Virusi vya UKIMWI.

Aidha, Majaliwa ametoa wito kwa wananchi,taasisi na asasi mbalimbali kuiishi kaulimbiu ya mwaka huu inayosema "Jamii Iongoze Kutokomeza UKIMWI" ili kuweza kufikisha Ujumbe kwa jamii kuhusu ushiriki kikamilifu kwenye upangaji mikakati na utekelezaji wa afua za kudhibiti UKIMWI.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn