logo

RAIS SAMIA ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 2,244 NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Disemba 09,2023 ametoa msamaha kwa wafungwa takribani 2,244 ambapo wafungwa 263 wataachiwa huru leo tarehe 09 mwezi Disemba, 2023, wafungwa wawili (2) waliohukumiwa adhabu ya kifo wamebadilishiwa adhabu ya kifo na kuwa kifungo cha maisha na wafungwa 1,979 wamepunguziwa sehemu ya adhabu zao ambazo wataendelea kuzitumikia gerezani.

.

Dkt.Samia ametoa msamaha huo ikiwa leo ni Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na mamlaka aliyopewa chini ya Ibara 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika msamaha huo, wafungwa walioachiwa ni wale ambao wote wenye sifa stahiki wamepunguziwa robo(1/4)ya adhabu baada ya kutoa punguzo la kawaida la moja ya tatu(1/3)linalotolewa chini ya kifungu cha 49(1) cha sheria ya Magereza sura ya 58. wafungwa hao ni wale waliohukumiwa kifungo kuanzia miaka miwili na kuendelea na ambao wametumikia robo(1/4)ya adhabu zao gerezani na ambao waliingia gerezani kabla ya tarehe 12 Oktoba,2023 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika sharti la 2(i -x);

.

Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu au sugu ambao wapo kwenye hatua ya mwisho (Terminal Stage). Ugonjwa na hatua hiyo vimethibitishwa na jopo la waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa, Mkoa/Mganga Mkuu wa wilaya.

.

Wafungwa wa maisha ambao wametumikia vifungo vyao kwa muda wa miaka kumi na tano (15) na kuendelea. Aidha kwa wafungwa wote waliobadilishiwa adhabu (commuted) hesabu zao zihesabike kuanzia tarehe ya kubadilishiwa adhabu.

.

Aidha,Rais Samia amesema ni matumaini yake wafungwa walioachiliwa huru leo tarehe 09 mwezi Disemba,2023 watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa taifa letu na kwamba watajiepusha kutenda makosa Ili wasirejee tena gerezani.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn