logo

MHANDISI NDOMBA: E-GA TUPO TAYARI KUFANYA KAZI NA TAASISI ZOTE ZA UMMA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya

Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi. Benedict Ndomba amesema mpaka hivi sasa jumla ya taasisi za umma 109 zimeunganishwa katika mfumo wa GovESB na mifumo imesajiliwa, na miongoni mwa taasisi hizo ni mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA),Wakala wa leseni za Biashara (BRELA), Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA)nk.

.

Mhandisi Ndomba ameyasema hayo leo Disemba 22,2023 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma.

.

Amesema mfumo wa GovESB umeleta mafanikio katika sekta za elimu na sheria kwani taasisi nyingi katika sekta hizo zinabadilishana taarifa kupitia GovESB.

"Kwa upande wa sekta ya sheria, taasisi zinazobadilishana taarifa ni mahakama, Jeshi la Polisi, Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) na ofisi ya taifa ya mashitaka (NPS). Hivyo mfumo huu umesaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi,uwazi pamoja na utoaji haki kwa wananchi kwa wakati" alisema mhandisi Ndomba.

.

Mkurugenzi huyo amesema ili kuhakikisha taasisi nyingi zaidi zinajiunga na mfumo wa GovESB na kubadilishana taarifa, e-GA imekuwa na mikakati madhubuti ikiwemo kufanya vikao na taasisi mbalimbali ambapo kati ya Agosti na Novemba 2023, e-GA imefanya na taasisi 55.

Amesema hapo awali ili mifumo ya TEHAMA iweze kusomana,ililazimika kuunganisha mfumo mmoja kuzungumza na mifumo mingine kila inapohitajika yaani "point-to-point connections",uunganishwaji huo ulisababisha urudufu wa mifumo,kupungua kwa usalama, kupunguza ufanisi wa mifumo na kuongeza gharama za usimamizi na uendeshaji wa mifumo ya TEHAMA.

.

"Kupitia GovESB, changamoto hizo zometatuliwa na sasa taasisi zote zinazobadilishana taarifa kupitia GovESB hupata taarifa zinazohitaji kwa wakati na kwa usalama zaidi" Alisema.

.

Aidha, Mhandisi Ndomba amesema mamlaka hiyo ipo tayari kufanya kazi na taasisi zote za umma ili kuhakikisha taasisi hizo zinajiunga na kubadilishana taarifa kupitia GovESB.

.

"Nitoe wito kwa taasisi zote ambazo bado hazijajiunga, kuwasiliana na e-GA ili ziweze kuunganishwa. Upo utaratibu wa kuwezesha mifumo ya taasisi za sekta binafsi inayohitaji kubadilishana taarifa na mifumo ya Serikali na kazi hii Itaendelea kutekelezwa kadiri ya

mahitaji". Alisema Ndomba.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn