logo

MAAFISA USALAMA BARABARANI WAAGIZWA KUDHIBITI AJALI KUELEKEA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Jumanne Sagini (Mb) amewaagiza maafisa wa usalama Barabarani kushuka chini kudhibiti ajali kuelekea sikukuu za Christmas na mwaka mpya.

Mheshimiwa Sagini ameyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mara ambapo amesisitiza kuwa, tangu Serikali iliporuhusu magari ya abiria kusafiri masaa 24 mpaka sasa taarifa inaonesha hakuna ajali mbaya ya gari iliyotokea.

"Tulisema basi linaloenda mwendo zaidi ya masaa 8 lazima iwe na madereva wasiopungua wawili ambao wote wanazingatia sheria za barabarani na tumeimarisha doria za mchana na usiku pia, niagize Maafisa wa ngazi za juu wa Kikosi cha Usalama Barabarani washuke chini wahakikishe madereva wanapimwa vileo, wanazingatia mwendo uliowekwa na hapa sio kwa gari za abiri tu ni kwa gari zote". Alisema Mhe.Sagini.

Aidha, Mhe.Sagini alisema kuwa utaratibu wa ukaguzi wa vyombo vinavyosafirisha abiria utakuwa ni endelevu.

Amesema kwa msimu wa sikukuu za mwaka jana yaani 2022 hapakutokea matukio mabaya ya ajali hivyo Serikali inatarajia msimu huu pia kuwa kama mwaka jana.

Aidha,aliwataka Wananchi kuhakikisha wanasherehekea kwa amani na utulivu, sambamba na kujiepusha na matukio yoyote ya kihalifu yanayoweza kuleta dosari nyakati hizi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn