MWIGIZAJI LEE SUN KYUN AFARIKI DUNIA
Mwigizaji wa Korea Kusini Lee Sun Kyun, ambaye alipata umaarufu kwa kazi yake katika "Parasite," aligundulika akiwa amefariki ndani ya gari lake katika wilaya ya Seongbuk ya Seoul mnamo Desemba 27.
Wahudumu wa afya waliripotiwa kumpata bila kuitikia, na polisi wa eneo hilo walishuku huenda akawa amejiua.
Habari hiyo ya kusikitisha ilifuatia mara baada ya uchunguzi wa matumizi ya dawa za kulevya, na siku moja kabla ya kifo chake, Lee Sun Kyun alikanusha kujihusisha na matumizi ya dawa ngumu.
Mapema mwezi Oktoba, alikabiliwa na shutuma za matumizi haramu ya dawa za kulevya.
Polisi walipata 'briketi za mkaa' kwenye gari lake, na kupendekeza mbinu inayoweza kuwa ya kujiua.
Lee Sun Kyun, mwenye umri wa miaka 48, alikuwa na kazi kubwa katika tasnia ya burudani ya Korea Kusini, akiigiza katika project mashuhuri kama vile "My Mister" na "Coffee Prince."
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

