MRADI WA MAJI NZUGUNI JIJINI DODOMA WAFIKIA ASILIMIA 96 - MHANDISI ARON JOSEPH
Kamati ya Kudumu ya Bunge, Uwekezaji ya Mitaji ya Umma (PIC) imeipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Dodoma (DUWASA) kwa utekelezaji wa mradi wa Maji wa Nzuguni Jijini Dodoma ambao unatarajia kukamilika mwaka huu 2024 na kwenda kupunguza tatizo la maji kwa wananchi katika eneo hilo.
.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Deus Clement Sangu (Mb) kwa niaba ya wajumbe wa Kamati,ametoa pongezi hizo leo January 28,2024 mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea mradi huo uliopo katika kata ya Nzuguni,Dodoma.
.
Mhe.Sangu amesema mradi huo unatekelezwa kisasa zaidi na wameona mfumo mpya ambao unaotumika katika mradi wa kutumia TEHAMA katika uendeshaji wa shughuli zote za visima kuanzia kujaza maji,kutibu maji na kupima kiwango cha maji ambao kitaalamu unaitwa SKADA.
.
"Ni mfumo wa Kompyuta tumeuangalia pale, ambao kwakweli umetupa imani sisi kama Kamati. Kilio kikubwa ambacho tumekuwa tukikipigania ni Mamlaka za Maji kama DUWASA zina uwezo wa ku-monitor hasa upotevu wa maji. Maji mengi yamekuwa yakizalishwa lakini hata namna ambavyo wanaweza wakajua kiasi gani kinapotea katika mifumo yao ni kazi" Alisema Sangu.
.
Mwenyekiti huo ametoa rai kwa mamlaka zingine za maji hapa nchini kwenda kujifunza namna DUWASA walivyotekeleza mradi huo ambao wao kama Kamati wanaona lina tija kubwa sana.
.
"Nimpongeze Mwenyekiti wa Bodi Menejimenti ya DUWASA kwa kazi kubwa, wanafanya kazi kubwa, sisi kama Kamati tunabeba jukumu moja la kwenda kuwapigania bungeni, tunaona fedha zilizotoka Shiling Bilioni 3.3 Kuna fedha DUWASA wanadaiwa hapa, ulitakiwa mradi ukamilike tarehe 15 mwezi January 2024 lakini wameshindwa kukamilika kwa sababu ya fedha hazijafika" alisema.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph amesema utekelezaji wa mradi huo hadi sasa wameweza kufikia asilimia 96, na mradi huo ulikuwa unatekelezwa na wahandisi (Wazabuni) Saba.
.
"Lengo la mradi huu ilikuwa tunataka kuhakikisha tunaongeza uzalishaji kutoka lita Milioni 68.6 hadi kwenda kwenye lita Milioni 76 (sawa na ongezeko la asilimia 11.7). Alisema Mhandisi Aron.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

