MSIWABEBESHE MZIGO WATOTO, FUATENI MTAALA WA ELIMU UNAVYOSEMA- PROF.MDOE
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe amewataka walimu wa madarasa ya awali kufundisha watoto kwa kufuata mtaala na siyo kuwafundisha masomo mengi yanayowalazimu kubeba mzigo wa begi la madaftari unaoweza kuwaletea athari siku za baadaye.
"Kwenye baadhi ya shule huko,tunawabebesha watoto mzigo mkubwa kuliko umri wao unakuta mtoto wa chekechea amebeba begi la madaftari 10 au 15 mpaka anapata kibyongo,halafu anajazwa materials kibao unamfundisha mtoto wa darasa la awali hadi vitu vya darasa la saba.
.
"Walimu walioandaliwa vizuri, vinara wa elimu ya awali hawawezi kufanya. mtaala wetu upo vizuri sana, fuateni mtaala kama ulivyo tusiwabebeshe mizigo isiyowahusu, wasioweza kuibeba " alisema Prof.Mdoe.
.
Amesema walimu hao wanapaswa kuwafundisha watoto kwa kuwalea kwa sababu ndio kipindi ambacho wanakua ili waweze kuwa watoto wazuri walioandaliwa vizuri kwa ajili ya kujiunga na elimu ya shule ya msingi.
.
"Ninyi kama walimu mna jukumu la kuwalinda watoto, mnafahamu changamoto zilizopo mtaani zinawatokea huko kwenye shule kama vile unyanyasaji wa kingono kwa watoto wetu mkiwa marafiki wa hawa watoto, wanakuwa wawazi kwenu" alisema Prof.Mdoe.
.
Kwa upande mwingine, Naibu Katibu Mkuu amewataka washiriki wa mafunzo ya Walimu wa shule za Awali kuhakikisha wanawaandaa vyema watoto wote ili hapo baadae tuweze kupata mtanzania aliyeelimika katika taifa letu.
.
Aidha, Prof.Mdoe amewasihi washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia yale ambayo watakayofundishwa ili kwenda kuwafundisha wengine na wao waweze kupata mafundisho hayo.
.
Kwa upande Mkurugenzi Mkazi wa Children in Crossfire, Craig Ferla amesema kwa tafiti zilizofanya na Chuo Kikuu UDOM mwaka 2023, inaonesha ya kwamba halmashauri 2 za wilaya ya Chamwino na Kongwa watoto katika darasa la awali wamefanya vizuri zaidi katika vipimo vyao Vya utayari wa shule, ukilinganisha na halmashauri zingine zenye mazingira yanayofanana.
.
Craig amesema kwa hivi sasa wapo mbioni kuhalalisha iwe elimu ya awali bora kwa mkoa mzima wa Dodoma
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

