logo

WATANZANIA TUJENGE UTAMADUNI WA KUTALII HIFADHI YA TAIFA KATAVI -AFISA UHIFADHI MSUYA

Imeelezwa kuwa Hifadhi zilizopo kusini mwa Tanzania zina vivutio vingi lakini hazina umaarufu mkubwa kama zingine Hifadhi nyingine hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Afisa Uhifadhi daraja la pili Bi.Beatrice Msuya Februari 28,2024 wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo ambapo amesema hifadhi ya taifa ya Katavi pamoja na kutokusikika masikioni mwa watu wengi lakini imesheeni vivutio vingi.

Amesema vivutio hivyo kuwa ni makundi makubwa ya wanyama kama vile simba,tembo,nyati nk. na pia kuna ziwa zuri na la kipekee ambalo limesheheni viboko,mamba na samaki aina ya kambale na kamongo.

"Hifadhi yetu ina sifa ya kuwa na viboko wengi kuliko hifadhi zingine hapa nchini, kwa wingi huo inaiweka kuwa hifadhi namba moja kwa viboko wengi." alisema Msuya.

Msuya amesema kupitia ziwa hilo kuna utalii wa uvuvi wa samaki (spot fishing)

ambao umekuwa ni sehemu ya kuwachangamsha watalii wanaotembelea hifadhi hiyo na wamekuwa wakifanya hivyo kwa kushindana kupata samaki mwenye uzito mkubwa kuzidi wengine.

Ameongeza kuwa utalii huo wa uvuvi umekuwa chachu kwa hifadhi hiyo ambapo samaki waliovuliwa na kupimwa kisha uachiliwa na kurudi ziwani.

Afisa Uhifadhi huyo amesema shughuli za uhifadhi ndani ya hifadhi hiyo zinahusisha kutambua mila na tamaduni za eneo hilo la Katavi.

"Ifikapo Julai wakazi wa Katavi huja hapa kufanya mambo yao ya mila na sisi tunawapa vibali vya kuingia ndani ya hifadhi kitendo hiki kimekuwa kivutio kwa baadhi ya watalii pia kinatusaidia kutunza mazingira" alisema Msuya.

Aidha, Msuya amewataka watanzania kujenga utamaduni wa kutalii haswa kwenye hifadhi ya Taifa Katavi kwa sababu ina upekee wa aina yake Tanzania.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn