logo

TANAPA IMEKAMILISHA MATENGENEZO YA BARABARA ZA HIFADHI YA TAIFA SERENGETI -MOBHARE MATINYI

Mkurugenzi wa Idara ya

Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Mobhare Matinyi amesema kuwa TANAPA katika hatua za awali imekamilisha matengenezo na sasa barabara za Hifadhi ya Taifa ya Serengeti zenye jumla ya kilomita 3,176 zinapitika na watalii wanaendelea kupata huduma zinazostahili.

"Hakuna changamoto kubwa iliyotokea kwenye upande wa viwanja vidogo vya ndege saba vilivyopo zaidi ya maji kujaa kwenye baadhi ya maeneo ya kuegeshea ndege. Hivyo baada ya maji hayo kukauka, huduma ziliendelea kwa usalama" alisema Matinyi.

.

Bw.Matinyi ameyasema hayo Machi 10,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari juu ya Maendeleo ya Utalii na Miundombinu Baada ya Mvua Kubwa ya El Nino katika Hifadhi ya Taifa Ya Serengeti Jijini Dodoma.

.

Amesema Hifadhi ya Serengeti ndiyo hifadhi yenye mtandao mrefu zaidi wa barabara ambazo ni za udongo ama changarawe na Barabara hizo zimegawanyika katika barabara kuu zilizo chini ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) na kundi la pili la barabara ndogondogo zilizo chini ya TANAPA yenyewe.

.

Mkurugenzi Matinyi amesema pale ilipotokea changamoto ya mvua za El Nino kulitokea mafuriko makubwa hifadhini kiasi cha kufunika barabara kuu zinazoleta watalii. Uharibu ulikuwa mkubwa.

"Hivyo basi, TANAPA ilichukua hatua za haraka za awali za kuzifanyia matengenezo barabara hizo ili kuhakikisha kwamba wageni wanaendelea kutalii na usafirishaji haukwami" alisema Matinyi.

.

Kwa upande mwingine, Matinyi amesema katika hatua za kati TANAPA inataka kunyanyua barabara nzima ya Golini-NaabiSeronera (km 68) kwa wastani wa sentimita 50 (nusu mita) kufuatana na ukaguzi uliyofanyika ili kuifanya iwe juu kidogo ya usawa wa ardhi, hivyo kuruhusu maji kutoka barabarani yapite kwenye mifumo ya mifereji na mitaro maji iliyopo pembezoni mwa barabara na kazi hiyo inaendelea.

.

Aidha, Matinyi amesema kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Februari 2024, watalii kutoka nje ya Afrika Mashariki ni 749,365, watalii wakazi (Expatriates) ni 10,531 na watalii wa Afrika Mashariki ikiwemo Watanzania ni 230,785.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn