logo

UHUMA FINANCIAL YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 1 KWA MWANAMKE MLEMAVU DODOMA

Meliana Mogwa, mama mzazi wa Agnes Steven (29), amewaomba watanzania msaada wa vifaa tiba pamoja na mahitaji mbalimbali kutokana na hali ya ulemavu aliyonayo mtoto wake ili aweze kumudu mahitaji ya kila siku.

Akizungumza wakati akipokea msaada wa shilingi Milioni 1 kutoka kwa Kampuni ya Uhuma Financial Services jijini Dodoma, Mogwa amesema Agnes anakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kitimwendo(Wheelchair) kwani hawezi kutembea hivyo inampasa mtu aweze kumsaidia kumbeba anapotaka kutoka nje ama kwenda mahali fulani, na Taulo za kike(Pedi) kwani amekuwa mtu asiweza kunyanyuka na kwenda popote.

"Mwanangu alipata ajali ya gari akiwa jijini Mbeya, nakumbuka ilikuwa tarehe 01 mwezi 2 mwaka 2020 ambapo ilipelekea kuumia sehemu za mgongo na kushindwa kutembea wala kusimama mpaka leo hii.

"Nawashukuru sana Uhuma Financial Services kwa msaada wenu, hii itatusaidia kutusogeza, nawaomba watanzania wenzangu msinichoke, muendelee kutusaidia ili mtoto wetu aweze kupona" alisema Bi.Meliana.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni hiyo, Mosha Juma, alisema wameguswa kumchangia Agnes kutokana na taarifa mbalimbali walizozipata kutoka kwa wananchi zikieleza uthubutu wa mwanamke huyo asiyekata tamaa licha ya kuwa katika hali aliyonayo lakini Bado anafanya biashara ya chipsi inayosaidia upatikanaji wa mahitaji ya familia akiwemo yeye, mwanae na mama yake mzazi.

"Sisi Uhuma Financial Services tulisikia kuhusu Agnes, changamoto yake na anavyoendesha maisha, tukaguswa kumchangia, biashara yake ina mtaji mdogo tumeamua kumuwezesha ili aweze kukuza biashara yake imsaidie katika kuendeleza mahitaji yake ya kiafya na kifamilia" alisema Mosha.

Nae, Agnes ameishukuru kampuni hiyo kwa kuguswa na changamoto aliyonayo, akiwaomba watanzania kuendelea kumsaidia katika Kila hatua anayoipitia.

Kwa mtu atakayeguswa kumsaidia Agnes Steven anaweza kuwasiliana naye kupitia namba yake +255746437929( jina MELIANA PAULO MOGWA)au unaweza kumchangia chochote kile ulichokuwa nacho.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn